HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 14, 2017

KIVUKO CHA MV. NYERERE KUFUNGWA INJINI MPYA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu, ametembelea na kukagua kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza na kujionea utendaji kazi wa kivuko hicho pamoja na changamoto zake.

Akiongea na watumishi wa kivuko hicho baada ya kujionea changamoto ya uendeshaji wa kivuko hicho, Dkt. Mgwatu alisema “tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia matengezo ya kinga kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo.”

Aidha Dkt. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko cha MV. Nyerere kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, pamoja na kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mgwatu alitembelea kivuko cha MV. Mara katika Mkoa wa Mara pamoja na kivuko cha MV. Ruvuvu katika mkoa wa Kagera na kujionea utendaji kazi wa vivuko hivyo pamoja na changamoto zake.
Kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Fundi wa kivuko cha MV. Nyerere akionyesha utendaji wa injini mojawapo ya kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Nyuma yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (wa pili kushoto) akiangalia utendaji kazi wa moja ya injini ya kivuko cha MV. Nyerere katika chumba cha mifumo ya kuendeshea kivuko hicho. Kivuko cha MV. Nyerere kinatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Kivuko cha MV. Mara kinachotoa huduma kati ya Iramba na Majita mkoani Mara.
Kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika eneo la Rusumo Mkoani Kagera. Picha na Theresia Mwami.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad