HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 11 May 2017

MHE. KAIMU JAJI MKUU AMALIZA ZIARA YAKE, MANYARA AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA MANYARA

Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Hanang/Katesh pindi alipowasili katika Mahakama hiyo kwa lengo la kujionea hali ya utoaji haki nchini.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiongea na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Hanang, kushoto ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi.
 Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma alipokuwa akizungumza nao alipofika Mahakamani hapo kwa lengo la kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama hiyo.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera pindi alipomtembelea ofisini kwake mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (kushoto) akimueleza jambo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania pindi alipomtembelea ofisini kwake mkoani Manyara, katika maongezi yake Mkuu wa Mkoa huo, ameisifu Mahakama mkoani humo kwa kusaidia kupunguza mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Kiteto mkoani humo kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusiana na mgogoro huo.
Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Mkoa na Mahakama na kusisitiza muendelezo wa ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi. (Picha na Mary Gwera)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad