HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 10 May 2017

MECHI YA YANGA NA MBEYA CITY SASA KUPIGWA SAA 12 JIONI

Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Yanga Salum(kulia).

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MCHEZO wa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara baina ya Yanga na Mbeya City unatarajiwa kufanyika kuanzia majira ya saa 12 badala ya saa 10 jioni kama ilivyozoeleka.


Akitoa taarifa hiyo Mjumbe wa kamati ya Utendaji Klabu ya Yanga Salum Mkemi amesema kuwa  mchezo huo utachezwa majira ya saa 12 kutokana na uwanja kuwa na shughuli zingine za michezo ambazo zitachelewa kumalizika.

Mkemi amesema kuwa wanapenda  kuwatangazia wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa soka jijini Dar es salaam sanjari na mikoa ya karibu kwamba; mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga SC na Mbeya City utachezwa uwanja mkuu wa taifa usiku badala ya kuanza saa 10:00 kama ilivyo ada. 


Mchezo huo utaanza majira ya saa 12:00 jioni kongwe kabisa nchini kucheza mchezo wake wa ligi kuu usiku katika miaka ya hivi karibuni.


Maamuzi haya yamezingatia matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu na hamu ya kuutazama mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa mchezo wa riadha itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo. 

Mkemi amewaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao kwani ulinzi utakuwa imara na thabiti.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad