HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 26, 2017

KIBAHA YAZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI

 Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha

WILAYA ya Kibaha imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na kuchagua viongozi wake watakaoongoza katika kipindi cha miaka mitano. Jukwaa hilo limempitisha Betty Msimbe kuwa mwenyekiti huku Sada Duda akichaguliwa katibu kipindi hicho .

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Leah Lwanji aliwataja viongozi hao ambao wamechaguliwa na akina mama wajasiriamali mbalimbali. Alieleza kuwa kuundwa kwa jukwaa hilo kutasaidia kuwezeshwa vikundi vya akinamama wajasiriamali kirahisi .

Leah alisema wanawake waungane waache kujiweka binafsi ili kupiga hatua kimaendeleo na kiuchumi. Hata hivyo alisema ,katika kipindi cha mwezi april hadi may mwaka huu halmashauri ya Mji huo imechangia sh .mil 56 kwa kukopesha vikundi 34 vya wanawake ,kwenye kata 14 zilizopo mjini humo.
 Leah alielezea kwamba ,July hadi desemba mwaka 2016 ,walitoa mil .16 kwa vikundi Tisa na Jan - march mwaka 2017 wametoa mil.70 kwa vikundi 46. Alisema kwa upande wa fungu la vijana afisa maendeleo huyo ya jamii ,wametoa asilimia kumi katika mapato ya ndani kwa kutoa sh.mil 32 zilizopelekwa saccos ya vijana .

"Tunamkabidhi mkuu wa wilaya ya Kibaha hundi ya sh.mil 56 kutoka NMB itakayogawiwa katika vikundi 34" alisema Leah .

Nae diwani wa viti maalum Mji wa Kibaha ambae pia ni katibu wa jukwaa la uwezeshaji mkoani Pwani ,Elina Mgonja alisema ,umoja wao utawawezesha kuwa na sauti kupigania fursa za kiujasiriamali. Alisema wamejipanga kuthubutu kuanzisha miradi mbalimbali na kushikana mkono ili kujikwamua kimaisha. Elina alitoa rai kwa wanawake kujitambua na kijithamini .
Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ,aliwataka wanawake wathubutu kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa kwenda na sera ya uchumi wa viwanda .

Aliwaomba wajenge tabia ya kugombea nafasi za uongozi bila kuwaachia wanaume. Assumpter alisema akinamama waamke waache kulala kwani sio wakati wa kuzorota. Alikemea tabia ya kusemana ,majungu na kukatishana tamaa .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad