HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 1, 2017

JAMII YATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UPIMAJI WA ARDHI.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimkabidhi mkazi wa Lamadi, Mama Juma hati miliki ya eneo lake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Lamadi juu ya kuwa na hati miliki ya maeneo yao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifurahia jambo na wakazi wa Lamadi.


Na Shushu Joel,BUSEGA.
JAMII imetakiwa kuchangamkia fursa zinazoendelea kutolewa na serikali katika ufanikishaji wa wananchi wote kupima maeneo yao ili waweze kuwa wamiliki halali kwa kupatwa hati za kumiliki maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya nyumba ya Makazi, Mh William Lukuvi alipokuwa akikabidhi hati halali za umiliki wa maeneo kwa wakazi wa kata ya lamadi,wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Unapopimiwa eneo lako unakuwa na faida nalo kubwa sana ambalo kwa sasa ni vigumu kuiona na hii ni kutokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uthamani ya kumiliki wa hati ya eneo.

“Unapokuwa na hati ya kiwanja chako au nyumba yako unakuwa na thamani kubwa na hii ni kutokana na kuwa unaweza ukauaga umasikini kwa kukopesheka na mabenki mbalimbali na hivyo kuwa na mtaji wa kufanya biashara zako bila kuwa na usumbufu wa aina yeyote ile” alisema Mh Lukuvi.

Aliongeza kusema kuwa hati hizi nilizo zikabidhi iwe ni changamoto kwa wale waliokuwa wakiwaona maafisa ardhi wangu wakipima maeneo na kuona kama vile ni utani sasa kazi mmeiona nah ii iwe fundisho kwa wale wasiopenda kuamini mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.

Aidha Waziri Lukuvi ameongeza wiki nne kwa maafisa Ardhi kumaliza kazi katika kata hito ua lamadi ili waweze khamia sehemu zingine kwani ambao bado waliokuwa awajapimiwa watapimiwa haraka ili kazi hiyo iweze kumalizika katika kata hiyo.

Kwa upande wake Afisa Ardhi Mteule wa wilaya ya Busega Magesa Magesa amemuhakikishia waziri Lukuvi kuwa ni lazima Busega yote ipimwe na wananchi kupatiwa hati za umiliki wa maeneo yao.

Aliongeza kuwa tulianza na lamadi nah ii ni kutokana kuwa kata hii inawakazi wengi kuliko kata zingine zote katika wilaya ya Busega.

Kwa upande wao walio kabidhiwa hati za umiliki wa maeneo yao wanesema kuwa waliokuwa wanabeza sasa wamekiona cha moto kwani waziri katukabidhi hati zetu halali za umiliki wa maeneo yetu na sasa tunao uwezo wa kukopesheka na kupata mitaji.

Musa Metusela ni mkazi wa lamadi na mfanyabiashara mkongwe katika eneo hilo anaeleza kuwa awali alikuwa akipata mkopo lakini si mkubwa wa kuweza kukidhi mahitaji yake ingawa nyumba yake inauweza wa kukopeshwa hata milioni 100 lakini kutokana na kutokuwa na hati ilimbidi apewe kiasi kidogo cha mkopo.

Alisema kuwa kwa sasa anaweza kupata mkopo mkubwa kutokana na kupata hati ya umiliki wa eneo lake.

Bi Joyce Magige ambaye ni mama wa watoto 4 aliyefiwa na mume wake miaka ya nyuma anasema kuwa sasa biashara zake zitafanyika nah ii ni kutokana na kuwa na uhakika wa kupata mkopo kutoka katika tasisi za kifedha kwani nyuma alikuwa anapata wakati mgumu kutokana na kutokuwa na umiliki wa eneo leke.

Aidha amempongeza waziri Lukuvi kwa kuwakabidhi hati zao kwani kuna baadhi ya wananchi waliokuwa wakiwacheka kwa kudai kuwa pesa zao zimeliwa na maafisa ardhi,sasa wamejionea wenyewe kuwa serikali ya JPM si ya ubabaishaji.

Aidha amewataka wananchi kutokuwa na tabia ya kusikiliza maneno ya watu wasio na mawazo mazuri kwani hao ni sawa na wale wanao kwamisha maendeleo ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad