HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 3 May 2017

“HALI YA DAWA NCHINI IMEIMARIKA”-MHE.KIGWANGALLA

  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.

“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.

Amesema kuwa katika kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Aidha hadi kufikia Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

Kufuatia Ongezeko ilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika sana.

“Hadi kufikia tarehe 15 Januari 2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216 kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad