HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 27 April 2017

YANGA KUIFUATA MBAO BILA NYOTA WAO WATATU WA KIMATAIFA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


MABINGWA watetezi wa kombe la Shirikisho la Azam HD Yanga wanaondoka jioni ya leo kuelekea Jijini Mwanz akwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo dhidi ya Mbao FC.

Yanga wanatarajia kuvaana na Mabo Jumapili ya April 30 katika Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa ni nusu fainali ya pili ambapo mchezo wa kwanza utakuwa  ni baina ya Simba na Azam utakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa Jumamosi.

Msafara wa wachezaji utaondoka majira ya saa 11 jioni smabamba na benchi la ufundi na viongozi wakitumia usafiri wa anga kwa ndege ya shirika la ndege la ATC.

Wakitoa taarifa hiyo kupitia Kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu hiyo, msafara wa wachezaji wa Yanga utakuwa na jumla ya wachezaji 21 huku wakiendelea kuwakosa noya wao kadhaa akiwemo Mzimbabwe Donald Ngoma, Vicent Bossou, Justine Zullu walio majeruhi, Malimi Busungu, Pato Ngonyani na Yusuph Mhilu.

Wachezaji watakao ondoka ni Makipa ni 

Deogratius Munishi ,Beno Kakolanya na Ally Mustapha. Nafasi ya ulinzi ni ; Nadir Haroub,Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani. 

Katika nafasi ya viungo ni pamoja na 

Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na Emmanuel Martin. 

Upande wa safu ya washambuliaji itaongozwa na ni Amissi Tambwe , Matheo Antony na Obrey Chirwa.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad