HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 13 April 2017

UCHAGUZI DRFA WAFANYIKA, KASONGO ATETEA KITI CHAKE

Mwenyekiti wa  chama cha Mpira mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Almas Kasongo (Kushoto).

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UCHAGUZI wa chama cha Mpira mkoa wa Dar es salaam (DRFA) umefanyika leo na kuwapata viongozi waoya huku Mwenyekiti Almas Kasongo ameendelea kutetea nafasi yake katika chama .

Katika uchaguzi huo Kasongo amefanikiwa kushinda .wa kuibuka na kura 12 dhidi kura 9 za mpinzani wake wakaribu Peter Muh

Salum Mwaking'anda ameshinda nafasi ya  makamu mwenyekiti huku nafasi ya katibu akichukua Msanifu Kondo.

Baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo alipata wasaa wa kuzungumza na kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi Kasongo amewashukuru wajumbe wa kamati ya utendaji kwa imani kubwa waliyonayo juu yake kwa kumchagua tena kwa awamu ya pili na kuahidi kuleta maendeleo ya soka la Dar es Salaam.

"Napenda kuwashukuru sana  wajumbe wote  kwa kuweza kuonyesha imani kubwa kwangu na mmeweza kuniamini tena katika awamu ya pili na ninaahidi katika miaka minne mingine kwa kushirikiana na wenzangu tutaendelea kuinua soka la Dar," alisema Kasongo.

Katika nafasi zingine Mchambuzi wa masuala ya soka Shaffih Dauda ameweza kuchaguliwa kuwa mjumbe mwakilishi wa vilabu huku Amour Amour, Bakari Mtumwa na Funua Ally wakichaguliwa kwenye kamati ya utendaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad