HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 14, 2017

Serikali kujenga Kituo cha Menejimenti ya Maafa Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake Nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 Dodoma, kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama.

Serikali imedhamiria kujenga Kituo cha Kitaifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura   kitakachosaidia katika kukabiliana, kuzuia na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea.

Hatua hiyo ya Serikali ya kuanza  kujenga kituo hicho katika eneo la Miuji mjini Dodoma inakuja huku  idadi kubwa ya wakazi ikiwa inaongezeka kutokana  na Wizara na baadhi ya Taasisi zake  kuhamia huko.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama alipokuwa akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha Makaridio na matumizi ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 mapema mwisho mwa wiki hii Bungeni Dodoma.

 “Kwa kutambua umuhimu wa kuwa na kituo hicho  cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Serikali  inaamini pindi kitakapokamilika kitakuwa na  msaada mkubwa  kitaifa katika kuokoa  maisha ya watu na mali zao’’ alisisitiza Mhagama.

Pamoja na hilo waziri alieleza tayari wadau mbalimbali wameanza kujitokeza na kuunga mkono hatua hizo ikiwemo Ubalozi wa Israel walipofanya ziara kujionea eneo husika na kuonesha nia ya kuunga mkono jitihada hizo.

“Tayari Washirika wa Maendeleo wameshajitoa na kuonesha nia ya kusaidia ambapo walikuja na kuongea na Ofisi ya Waziri Mkuu na kutembelea eneo hilo.”Alisema waziri Mhagama. Aidha Ofisi ya Waziri Mkuu imeshatenga fedha na kubaini mipango ya kusaidia kutekeleza ujenzi wa kituo hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akichangia hoja wakati wa kujadili makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017, aliyekaa ni Naibu wake (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezana na baadhi ya Watendaji wa Ofisi yake mara baada ya Kupitishwa kwa makadirio ya Bajeti ya ofisi yake kwa mwaka 2017/2018 Dodoma Aprili 11, 2017.
baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa na nyuso za furaha baada ya Bajeti yao kupitishwa Bungeni Dodoma Aprili 11, 2017. katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na wakwanza kulia ni Naibu wake Mhe. Antony Mavunde. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU -DODOMA)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad