HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 21 April 2017

POVU LAMPONZA MANARA, APELEKWA KAMATI YA MAADILI NA TFF

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baada ya kutoa kauli zisizo nzuri kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) na kuitupia shutuma mbalimbali hatimaye kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo limefanya maamuzi ya kumfikisha Msemaji wa Simba Hajji Manara mbele ya kamati ya maadili.

TFF imeweka wazi kuwa kila mwanafamilia wa mpira wa miguu Tanzania analazimika kuheshimu na kufuata kanuni za maadili za shirikisho kama zilivyoainishwa kwenye kanuni zake mbali mbali.

Katika Mkutano wa klabu ya Simba uliofanyika siku chache zilizopita ukiongozwa na msemaji wao Manara ulitoa shutma kwa TFF kuwa hauwatendei haki na una mpango wa kudhulumu haki yao na hata hivyo miaka minne ya Rais Jamal Malinzi umedhamiria kuhakikisha Simba hawachukui ubingwa.

Manara alizidi kutoa shutuma kwa Rais wa TFF na kusema kuwa wanajua mahusiano yake na mwamuzi Jonesia Rukyaa ambaye alikuwepo katika kutoa ushahidi mbele ya kamati ya Katiba,Hadhi na wachezaji wakati wa kupitia hukumu ya saa 72 iliyotoa maamuzi ya Simba kupewa alama 3 na goli 3 dhidi ya Kagera baada ya kumchezesha Mohamed Fakhi akiwa na kadi za njano.

Ili kutunza heshima ya mpira wa miguu Tanzania, wanafamilia wa mchezo huo katika kutimiza masharti ya kanuni za maadili za TFF, hawana budi kuheshimu na kufuata taratibu zote hizo ndani na nje ya uwanja.

Taswira njema ya shirikisho inajenga imani ya wadau wakiwamo serikali, mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, vyombo vya habari, vyama vya mpira vya kimataifa, NGO’s na watu binafsi kwa taasisi (TFF). Kinyume chake ni kulibomoa shirikisho. Dhima ya uongozi wa TFF ni pamoja na kulinda na kutunza heshima hii. Hivyo vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uvunjaji wa maadili havitavumiliwa, na vikitokea hatua zitachukulia.

Na kwa muktadha huu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, limemfungulia mashtaka ya kinidhamu Msemaji wa Simba Bw. Hajji Manara kwenye Kamati ya Maadili. Na leo hii Aprili 21, 2017 atapewa mashtaka yake na kujulishwa lini na wapi yatasikilizwa. TFF inaendelea kutoa rai kwa wadau wa mpira kuwa pamoja ni kwamba ni haki yao kushauri, kupendekeza, kukosoa lakini yote haya yafanyike kwa staha ili kutunza heshima ya mpira wetu.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad