HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 25 April 2017

NEEMA KWA WATU WENYE ULEMAVU TANZANIA KUPITA MRADI JUMUISHI KWA WOTE

Mradi “Jumuishi kwa wote” (All Inclussive) ni jitihada za wadau kuwawezesha watu wenye ulemavu kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi, na kiafya. Mradi huu umezinduliwa Aprili 21, 2017 Jijini Dar es salaam katika viwanja vya michezo kwa vijana vya J. M. Kikwete. Uzinduzi huo umefanywa na Kamishna Msaidizi Idara ya Ustawi wa Jamii Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Bi. Josephine Lyangi.

Tukio hilo lilihudhuriwa na wadau mbali mbali wa maendele nchini akiwemo balozi wa Itali nchini, Roberto Mengoni ambaye alisisitiza kusaidia miradi ya kijamii kama hii, Balozi Mengoni aliwakilisha shirika la kitaliano la ushirikiano wa kimaendeleo ambalo ndio mdhamini mkubwa wa mradi huu.
Mwakilishi wa CEFA Tanzania bwana Dario ameeleza kuwa mradi huo wa wa Jumuishi kwa wote utagharimu euro  1,764936.00 ambazo ni takribani billion 4 shilingi za kitanzania. Mradi huu utakuwa na vipengele vikuu vitatu ambavyo ni Afya, uwezeshwaji kiuchumi pamoja na ushiriki katika shughuli za kijamii kama michezo pamoja na elimu. CEFA pamoja na washirika wenza  ambao ni CO.PE, CCBRT, IVREA sisters, ATE , COM.SOL na JMK YOUTH PARK watashiriki utekelezwaji wa mradi huu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mradi huu unalengo la kuwafikia watu wenye ulemavu zaidi ya elfu kumi na saba ambao watafaidika na mradi huu kutokana na kutoka na utekelezwaji wa majukumu mbalimbali. Shughuli kubwa mojawapo ni ujenzi wa kituo kikubwa na chakisasa cha watu wenye ulemavu, kituo hiki kinajengwa katika eneo la Kawe katika manispaa ya Kinondoni.


Mkurugenzi wa sera na utetezi wa CCBRT
Fredrick Msigallah akizungumzia 
malengo ya mradi.
Hii ni katika kuwapa nguvu walemavu na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kuajiriwa na kupewa nafasi za kufanya shughuli za kimaendeleo kama sharia ya  walemavu ya mwaka 2010 inavyosema “katika kila kampuni inayo ajiri zaidi ya watu ishirini 3% wanatakiwa kuwa ni watu wenye ulemavu.”

Takwimu za sense ya 2012 zinaonyesha kuwa idadi ya wakazi wa Jijini Dar es  salam ni 4,363,541  kati ya idadi hiyo asilimia 7% ni watu wenye ulemavu , pamoja  na kuwa na uwezo hafifu wa viungo  kufanya kazi  kama wengine  pia wamekuwa wakikumbana na  changamoto  na vikwazo mbali mbali  katika kupata huduma za afya, elimu pamoja  na ushiriki katika shughuli za kijamii hasa michezo.

Fredrick Msigallah  ambaye ni mkurugenzi kitengo cha sera na utetezi CCBRT hospitali ameeleza kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa kama mzigo katika famila zao kutokana na kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi na kuzalisha kipato katika familia zao. Bwana Msigalla ameongeza kuwa mradi huu utanufaisha watu wengi hivyo amesisitiza watu wenye ulemavu kuonyesha ushirikiano ili misaada hii iwafikie kirahisi.

Watu wenye ulemavu wanatakiwa kuto jiweka nyuma na kujiona kama hawafai na wasio kuwa na umuhimu katika jamii bali wanapaswa kutambua kuwani miongoni mwa jamii na wanatakiwa kushirikiana nayo katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo na kijamii.
Balozi wa Itali nchini bwana Roberto Mengoni akizungumza katika uzinduzi wa mradi (picha na Gabriele Fiolo).
Kamishna Msaidizi Idara ya Ustawi wa Jamii Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu, Bi. Josephine Lyangi akizungumza.
Wadau walio hudhuria uzinduzi wa mradi wa All Inclusive. (picha na Dinah Chuwa)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad