HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 7 April 2017

MKUU WA WILAYA YA MKURANGA AWAONYA VIJANA WA KIUME WANAOWAFUATA WANAFUNZI WA KIKE

 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akizungumza na wananchi na wanafunzi katika shule ya msingi Kazomla wakati uzinduzi wa kisima kirefu kilichojengwa na Africa Reflection Foundation.
 Mwakilishi wa Mbunge wa Mkuranga na Katibu wa Mbunge , Omary Kisatu akizungumza katika shule ya msingi Kazomla wakati uzinduzi wa kisima kirefu kilichojengwa na Africa Reflection Foundation.
 Mwasisi wa Africa Reflection  Foundation, Maryvone Pool akizungumza juu ya ufadhili wa visima  viwili katika shule za msingi Kazomla na Mkamba
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga pamoja na wafadhili wa mradi huo wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kisima katika shule ya Msingi ya Mkamba.
  Mkuu wa  Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akigawa galoni kwa wanafunzi watawekea wanafunzi maji wakati wanarudi majumbani mwao.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga akiwa katika picha pamoja na wanawake waliokabidhiwa mbuzi kwa ajili ya kukuza kipato leo katika wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Wananchi wa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga katika uzinduzi wa kisima kirefu kilichojengwa na Africa Reflection Foundation(.picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema wanafunzi wakipata mimba katika wilaya hiyo sheria itachukua mkondo wake kwa mwanafunzi pamoja na kijana wa kiume aliyehusika katika mimba hiyo.
Mkuu wa Wilaya , Sanga ameyasema hayo wakati akizingumza katika uzinduzi wa visima viwili katika shule za msingi za Kazomla na Mkamba vilivyochimbwa na Mfuko wa Afrika Reflection, amesema taifa linajengwa na watu waliosoma hivyo kuacha wanafunzi wakipata mimba ni kutengeneza taifa la mambumbu.
Sanga amesema juhudi zinazofanywa na mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega za kutafuta wafadhili wa kuchimba visima ni kutaka Mkuranga  kukua kielimu.
Amesema Mkuranga ni Wilaya yenye viwanda vingi ambapo wataalam wanahitajika lakini Mkuranga haina vijana wa kufanya kazi hizo hivyo ni lazima wanafunzi wasome kwa bidii.
Aidha amesema kuwa visima vilivyochimbwa vitumike kwa matumizi sahihi pamoja na shule kutengeneza bustani  za mboga mboga pamoja na matunda na shule kuwa mradi huo kutokana na mtaji wa visima hivyo.
Amesema visima hivyo vitunzwe na vitu vikiibiwa wananchi wote watawekwa ndani kutokana na kufanya uzembe wa kutolinda visima hivyo ambavyo wafadhiri wamejitoa.
Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wananchi kulima zao la muhogo kila mtu heka mbili kwani hakuna chakula cha msaada na kuongeza kuwa majani yanastawi kuliko mihogo na mazao mengine jambo ambalo haliwezi kukubalika wanachi washindwe kulima na kuzungukwa na majani yaliyositawi
Nae Mwasisi wa Africa Reflection  Foundation, Maryvone Pool  amesema kuwa wamechimba visima 100 katika Wilaya ya Mkuranga na wataendelea kuchimba visima kadri vitavyohitajika.
Maryvone amesema kuwa watu wanajitoa kwa misaada hivyo amewataka wanawake kujitoa katika kufanya kazi za kilimo na mazao yao watayatafutia masoko nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad