HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 7 April 2017

MAREKANI YASHAMBULIA KWA MAKOMBORA KAMBI YA JESHI LA SYRIAMarekani imefanya mashambulizi ya anga katika kambi ya jeshi la Syria katika kujibu mapigo ya tukio linalodaiwa kuwa shambulizi la silaha za kemikali dhidi ya raia katika mji unaoshikiliwa na waasi.Makombora 59 aina ya Tomahawk yamerushwa kutoka kwenye meli mbili za kijeshi kutoka bahari ya Mediterranean.Rais Donald Trump amesema wameshambulia kambi ya jeshi ya Shayrat ambayo ilifanya mashambulizi ya kemikali siku ya jumanne.Hili ni shambulizi la kwanza la Marekani moja kwa moja dhidi ya serikali ya Syria. Urusi ambayo inamuunga mkono rais Bashar al-Assad, imeshutumu shambulizi hilo.
                          Kambi ya jeshi ya Shayrat inavyoonekana baada ya mashambulizi 
                             Meli ya jeshi la Marekani ikirusha makombora ya Tomahawk

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad