HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 2, 2017

MAMA MJANE AJITOKEZA KWA VYOMBO VYA HABARI,AKIDAI KUDHULUMIWA NYUMBA ALIOACHIWA NA MUMEWE

Mjane Farida Saleh Amrani amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kulalamika kudhulumiwa nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mme wake aliyefariki mwaka 2011.

Akizungumza na kuonesha hati halali za nyumba hiyo yenye kitalu namba 2111 iliyopo Mbezi Beach Kata ya Maliasili, Farida alisema kuwa katika nyumba hiyo walihamia mwaka 2002 na hati ya nyumba hiyo ilikuwa kwa mwanasheria kipindi chote hata pale marehemu mumewe alipofariki.

Amesema kuwa, baada ya mume wake kufariki mtoto wa marehemu mkubwa aliambiwa afungue mirathi lakini akawa anasema taratibu za kabila la kihaya ni baada ya mwaka mmoja kumalizika.

Farida ameeleza kuwa, mumewe Alfred Kyoma alifariki akiwa safarini Bukoba na amemuacha na watoto wawili ambao baada ya kumalizika kwa msiba familia nzima walikubaliana nyumba ipangishwe ili fedha zitakazopatikana ziwasomeshe watoto,ambao mmoja yupo kidato cha tano sasa hivi na mwingine cha kwanza.

Nyumba hiyo kwa Yusuph Shaban Omari ambaye ni mmiliki wa Royal Village Hotel iliyopo Temeke na ameuziwa na kaka wa marehemu lakini katika hati ya mauzo ikidaiwa kuandikwa jina la Alfred Athanas Kyoma akishirikiana na mtoto wa Marehemu.

Majirani wa nyumba hiyo Wamesema kuwa siku chache zilizopita waliona watu wakivunja nyumba na kuingia ndani na kutoa vitu ndani vya mpangaji anayekaa hapo ambaye alikuwa amesafiri.

Kwa sasa nyumba hiyo imewekwa mlinzi ambaye jitihada za kumwambia afungue zilishindikana baada ya kugoma kuruhusu watu kuingia ndani,aidha inadaiwa kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa kiasi cha shilingi milion sitini (60).
⁠⁠⁠Mjane Farida Saleh Amrani akizungumza na waandishi wa habari akilalamika kudhulumiwa nyumba aliyoachiwa na mumewe aliyefariki 2011, ambapo inadaiwa kuwa kaka wa marehemu alibadili hati ya nyumba na kuiuza.
Hati halali iliyokuwa kwa mwanasheria ambapo marehemu alitoa maagizo ya kupatiwa mkewe kama likitokea tatizo lolote akabidhiwe mkewe.
Muonekano wa nyumba husika,ambayo Mlinzi alikwemo ndani lakini alikataa kufungua geti 
Baadhi ya Majirani wakijaribu kumwomba mlinzi afungue mlango ili waingie ndani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad