HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 2 April 2017

KAGERA SUGAR WAITEKETEZA SIMBA UWANJA WA KAITABA

Kiungo wa timu ya Simba James Kotei raia wa Ghana  ambaye anauwezo wa kucheza namba zaidi ya moja Uwanjani akipambana kupata mpira mbele ya wachezaji wa kagera Sugar leo hii uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.


Na Faustine Ruta, Bukoba

Timu ya soka ya Kagera Sugar imefanikiwa kuichapa timu ya Simba kwa jumla ya bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu bara ambapo baadhi ya wachambuzi wa soka wamesema kuwa kutokana na Kagera Sugar kuifunga Simba inawezekana ikawa ndiyo nafasi kwa Yanga kutetea ubingwa wao ambapo baada ya mchezo wa leo Simba wamebaki nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 55 huku Yanga wakijikita kileleni wakiwa na pointi 56 baada ya michezo 25 uliochezwa jana. 
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Kaitaba ulishuhudia timu ya soka ya Simba wakishindwa kutumia nafasi zao vyema walizopata na kujikuta wakifungwa bao 2-1.Magoli ya Kagera Sugar yalifungwa na Mbaraka Yusuph, goli la pili likifungwa na Edward Christopher huku goli la kufutia machozi kwa Simba sports Club likifungwa na Mzamilu Yasin dakika 61 ya kipindi cha pili. 
Kwa matokeo hayo Yanga wanaendelea kuwa kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na jumla ya pointi 56 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 55 huku Kagera Sugar wakifikisha jumla ya pointi 45 na kupanda hadi nafasi ya tatu huku nafasi ya nne ikishikiliwa na Azam wenye pointi 44.

Kikosi cha Simba kilichoanza
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza dhidi Simba ya Jijini Dar es salaam.
Mshambuliaji wa timu ya Simba Mrundi Laudit Mavugo akijaribu kumtoka Beki wa Kagera Sugar Juma Ramadhan .
Kichuya Akiambaa na Mpira
Meza kuu
Kikosi cha Kagera Sugar kikiomba kabla ya mtanange kuanza

Mbaraka akipongezwa kwa bao
Hadi mapumziko Simba walikuwa nyuma ya bao 1-0

Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wakiwa jukwaa kuu kabla ya mchezo wa Simba dhidi ya Kagera Sugar kuanza.
Mashabiki waliingia kwa wingi kwenye Mtanange huo ulikuwa na hamsha hamsha ya kila aina yake.
Winga wa timu ya Simba Shiza Kichuya akiambaa na mpira wakati mchezo ukiendelea
Kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla akiachia Shuti kali ambalo lilipanguliwa na Kipa Juma Kaseja

Simba walipata bao lao la pekee kipindi cha pili dakika ya 61 na mtanange kuwa 2-1
Nahodha wa timu ya Simba Jonas Mkude akitafakari baada ya timu yake kuchapwa bao 2-1 na Kagera Sugar.


Mecky Mexime Kocha wa Kagera Sugar akiwa amebebwa na Wachezaji wa Kagera mara baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.
Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mlinda mlango wao Juma Kaseja.
Mtanange ulipomalizika Kipa Kaseja alipewa zawadi kutoka kwa mashabiki wa Kagera Sugar pamoja na Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akikaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

CHANZO: BUKOBASPORT BLOG

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad