HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 9 April 2017

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU KUONGOZA KAMPENI YA KUNUSURU BONDE LA MTO RUAHA MKOANI IRINGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Kampeni ya kunusuru Bonde la Mto Ruaha Mkuu lililopo Iringa kutokana uharibifu mkubwa unaendelea, huku akiambatana na Mawaziri watano ambao watasaidia kuokoa uharibifu wa Mazingira.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Januari Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo Jijini Dar es salaam, amesema kuwa Ofisi hiyo imeanzisha Kampeni hiyo kwa sababu Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu ni kubwa kuliko yote hapa Afrika Mashariki.

Amesema kuwa uharibifu unafanywa kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika Bonde hilo unasababisha kukauka kwa Mto Ruaha ambao ni tegemezi katika nyanja za kiuchumi.

Aidha, Makamba amewataja Mawaziri watakaoongozana na Makamu wa Rais kuwa ni pamoja na Waziri wa Maji, Gerson Lwenge, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe, Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba.
Vile vile, ameongeza kuwa hali ya mazingira kwa sasa ni mbaya sana kwenye bonde hilo kwani ukifika wakati wa kiangazi mto huo wa Ruaha Mkuu hautirirshi tena maji kama ilivyokuwa zamani.

"Hali hii inasababisha kupungua kwa watalii, shughuli za kiuchumi na uzalishaji wa umeme ambao unamrahishia mwananchi wa kawaida kupata umema nafuu, pia uhalibifu huu wa Mazingira unahatarisha maisha ya wanyama,"amesema Makamba.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kutunza vyanzo vya maji, Mazingira ili viweze kuwaletea manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.​

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad