HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 3, 2017

MADHARA YA MITANDAO KIJAMII KIAFYA YAELEZWA

Wanasayansi wamethibitisha kuwa mitandao ya kijamii ndicho chanzo cha magonjwa mbalimbali yakiwamo ya akili na kulemaa kwa mishipa ya shingo.
Wanasayansi wanaeleza kuwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, whatsApp na instagram, ujumbe wa simu na michezo ya kwenye intaneti husababisha magonjwa ya akili, uraibu na kujeruhiwa kwa shingo na uti wa mgongo kunakosababishwa na kuinamia simu muda mrefu.
Tovuti ya Neck Institute (London) imeeleza kuwa madhara ya shingo na uti wa mgongo yanayosababishwa na matumizi ya simu kwa muda mrefu hasa kwa kuandika ujumbe mfupi au Text Neck Syndrome, huathiri mamilioni ya watu duniani.
Daktari bingwa wa neva za fahamu (neurologist) wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja amesema bado hakuna ushahidi wa kisayansi kama matumizi ya simu yanaathiri mishipa ya shingo, lakini namna ya matumizi yake yalivyo yanaathiri misuli.
Profesa Matuja amesema kuinamia simu muda mrefu kunasababisha maumivu ya mgongo, shingo na hata kichwa.
Daktari wa mishipa ya fahamu, wa Florida nchini Marekani, Dean Fishman amesema mishipa ya shingo hasa kwa sehemu ya nyuma huathirika kutokana na kuandika ujumbe mfupi kila mara na kwa muda mrefu, kwa sababu kitendo hicho kinamfanya mtumiaji kuiinamia simu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad