HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 5 April 2017

KESI YA MAUAJI YA DK. MVUNGI KUSIKILIZWA MAHAKA KUU

Na Karama Kenyunko

Jumla ya Mashahidi 30 wanatarajiwa kutoa ushahidi katika Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kufuatia kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk. Sengondo Mvungi.

Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali Patric Mwita ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  leo, baada ya kumaliza usiklilizwaji wa awali kwa kusoma ushahidi wa mashahidi thelesini mbele ya Hakimu Mkazi mkuu Thomas Simba.

Aidha wakili Mwita amedai kuwa wakati wa usikilizwaji pia vielelezo 13 vikiwemo, mapanga, bastola, postmortem ya daktari na hati ya ukamatwaji vitawasilishwa mahakamani hapo.

Jumla ya watuhumiwa 12 walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mwaka 2013 ambapo wanne waliachiwa huru huku mmoja akifariki dunia.

Watuhumiwa waliofutiwa kesi na kuachiwa huru baada ya DPP kuondoa mashtaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashtaki ni Hamad kitabu, Zacharia Msese na Masunga Makenza. Mshtakiwa aliyefariki alifahamika kwa jina la Chibago Chiuguta. 


Watuhumiwa ambao wanakesi ya kujibu na kesi yao itasikilizwa mahakama kuu baada ya kupangiwa tarehe ya kusikilizwa ni Chibago Magozi, Juma Mangungu, Paulo Mdonondo,  Mianda Mlewa, Msingwa Matonya.


Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo na John Mayunda.

Baada ya maelezo ya mashahidi kusomwa, washtakiwa wameileza mahakama kuwa watatotoa maelezo yao mbele ya wakili wao ambaye watepatiwa pindi wakifika mahakama kuu.
Kufuatia hayo kesi hiyo sasa inasubiri kupangiwa tarehe ya usikilizwaji (session). Washtakiwa wamerudishwa mahabusu.

Inadaiwa kuwa Novemba 3, mwaka 2013, huko Mbezi eneo la Msakuzi Kiswegere washtakiwa walimuua Dk. Sengondo Mvungi .

Walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Marehemu Mvungi alizikwa baadae kijijini kwao Chanjale Kisangara juu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad