HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 18 April 2017

KAMA ULIPITWA NA TAMASHA LA PASAKA, WAWEZA ONA HAPA HILICHOJILI HUKO

Waibaji wa kwaya ya Sauti ya Mungu kutoka Kanisa la Siloam, Mbezi, Makonde jijini Dar es Salaam, wakiimba na kucheza wimbo unaoitwa Mungu uliyetuumba wote, vizazi vyote katika Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk)  
Vijana wa Kwaya ya KKKT Mwananyamala, wakiimba na kucheza wimbo unaoitwa Siku ya Mwisho, wakati wa tamasha hilo.  
Mashabiki waliohudhuria katika Tamasha la Pasaka wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka na kupiga picha za selfi, uwanjani hapo. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama (kulia), akiimba sambamba na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Martha Mwaipaja, wakati akitumbuiza katika tamasha hilo. 
Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba, akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto), mara baada ya kumaliza kutoa hotuba yake. Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama. 
Wachungaji walioohudhuria tamasha hilo, wakimwombea mwimbaji, Solly Mahlangu (chini aliyepiga magoti), kutoka Afrika Kusini, wakati alipotumbuiza kwenye tamasha hilo jana jijini. 
Mwimbaji wa nyimbo za Injili, Martha Mwaipaja, akitumbuiza katika tamasha hilo. 
Vijana wa Kwaya ya KKKT Mwananyamala, wakiwa katika harakati ya kutumbuiza kwa wimbo unaoitwa Siku ya Mwisho, wakati wa tamasha hilo.  
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama (wa nne kushoto), akimkabidhi Tuzo aliyomtunuku Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba aliyeipokea kwa niaba yake, wakati wa tamasha hilo.  
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Solly Mahlangu wa Afrika Kusini akiimba na kuzirudi ngoma wakati alipotumbuiza katika tamasha hilo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana.  
Mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto), akicheza kijeshi jeshi sambamba na msanii Solly Mahlangu wa Afrika Kusini wakati alipotumbuiza katika tamasha hilo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana. 
Mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto), akicheza sambamba na msanii Solly Mahlangu wa Afrika Kusini wakati alipotumbuiza katika tamasha hilo, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad