HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 6, 2017

JSI WATOA ELIMU YA MALEZI KWA WATOTO WANAOISIHI MAZINGIRA MAGUMU WILAYA YA TEMEKE



Wadau wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI) wametoa mafunzo ya mfumo jumuishi kwa watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Mfumo huo umewekwa na serikali kwa kushirikiana na wadau kama WAMATA na (JSI) ili kutoa huduma kwa pamoja kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na sio kila mdau kwenda au kupeleka huduma kipekee

Akitoa mafunzo hayo Asia Jingu amesema mfumo huu ni muhimu kwani utawezesha kuweka taratibu za utoaji wa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na si kila taasisi ama mdau kuwa na utaratibu wake jambo ambalo lilikuwa likisababisha baadhi ya watoto kukosa huduma kutokana na sababu mbalimbali.

Pia Mfumo huu utahamasisha ushirikiano wa karibu kati ya wadau na taasisi zinazojihusisha na kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.



Asia Jingu pia amesema watoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanatakiwa kutoa huduma kwa uweledi mkubwa kwani kazi hii ni ya kujitolea,kwa hiyo kwa wale wote watakaopata mafunzo kwa ajili ya huduma hiyo katika Mitaa mbalimbali wawe waadilifu kwa watoto na pia kutoa huduma bila ubaguzi kwa watoto wala kutowadhuru watoto hao walio katika mazingira magumu.


Mkufunzi wa masuala ya malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi (JSI), 
Asia Jingu akitoa mafunzo hayo kwa viongozi mbalimbali,
watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.


watendaji na wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakiwa makini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad