HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 12 April 2017

JESHI LA POLISI LAPOKEA PIKIPIKI 20 KUTOKA KAMPUNI YA HUAWEI TANZANIA

 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Gaomeng Dong (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa makabidhiano ya pikipiki 20 zilizotolewa na Kampuni ya Huawei kwa Jeshi la Polisi nchini zitakazosaidia katika shughuli mbalimbali za kukabiliana na uhalifu hapa nchini. Pikipiki hizo ni sehemu ya pikipiki 56 zilizokuwa zimeahidiwa na Kampuni hiyo kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kusaidia ufanisi wa kazi kwa Jeshi hilo.

 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki akiwa amepanda kwenye moja ya pikipiki hizo alipokuwa akiijaribu, muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Gaomeng Dong (wa pili kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano hayo, iliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

 Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, D-IGP Abdulrahman Kaniki akizungumza katika hafla hiyo, 
Mkuu wa Maboresho wa Jeshi la Polisi nchini, DCP Goodluck Mongi akifafanua jambo wakati akielezea Maboresho ya Jeshi hilo, katika hafla fupi ya makabidhiano ya Pikipiki kati ya Kampuni ya Huawei na Jeshi la Polisi, iliyofanyika katika viwanja vya Polisi Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, SACP Suzan Kaganda akizungumza machache katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Gaomeng Dong akizungumza.
Sehemu ya pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa Jeshi la Polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad