HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 24 April 2017

Hoteli ya Essque Zalu Zanzibar yawataka Watanzania kuitembelea

Hoteli yenye hadhi ya nyota tano iliyopo Nungwi kisiwani Zanzibar ya Essque Zalu , mwishoni mwa wiki iliandaa chakula cha jioni ambacho kiliwaleta wapishi waliobobea kisiwani hapa pamoja huku ikiwataka Watanzani kuitembelea na kupata kilicho bora.

Hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyofana iliandaliwa na Jussi Husa kutoka hoteli ya Essque Zalu Zanzibar ambaye ni mmoja kati ya wapishi wakubwa kisiwani hapa na ambaye aliwaalika wapishi wengine wanne kuweza kutengeneza chakula kilichowafurahisha wageni waliohudhuria.

Wapishi waalikwa walioshiriki kuandaa chakula  ni pamoja na Chef Alan kutoka Double Tree Hilton, Lucas Wollman kutoka hoteli ya Kilindi, Ludek Munzar kutoka hoteli ya Tulia na  Bouya Jean Pascal Diedhiou kutoka Melia' hotel

Tukio hilo lililenga kuwaleta pamoja wapenzi wa vyakula mbali mbali.Jumla ya aina saba ya vyakula zilipikwa kwa ustadi wa hali ya juu na wapishi waliobobea visiwani hapa na wegeni waliweza kushiriki kwa pamoja

Kwa upande mwingine pia, tukio hilo lililenga kuwaweka pamoja wapishi na kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuongeza ubunifu katika huduma ya chakula ambayo ni sehemu muhimu ya utalii katika kisiwa cha Zanzibar.

Hoteli ya Essque Zalu Zanzibar ni moja kati ya hoteli ya nyota tano kisiwan I Zanzibar ambayo inatoa huduma mbali mbali zenye hadhi ya kimataifa kwa wageni wanaofika hotelini hapo.
Meneja mkuu wa hoteli ya Essque Zalu Zanzibar, Duarte Correia akizungumza kwenye hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika hotelini hapo mwishoni mwa wiki.
Mkufunzi kutoka chuo cha muziki Zanzibar, Heri Mohamed (kulia) akitoa mafunzo ya kupiga ngoma za asili kwa wageni waliohudhuri hafla ya chakula cha jioni katika hoteli ya Essque Zalu Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni wakibadilishana mawazo na mwenyeji wao, Meneja mkuu wa Zalu Hotel Duarte Correa (wa kwanza kulia) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika hotelini hapo mwishoni mwa wiki.
Wapishi waliobobea katika aina mbali mbali ya mapishi ya vyakula wakiandaa aina maalum ya chakula mezani tayari kwa ajili ya kuliwa na waalikwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika katika hoteli ya Essque Zalu Zanzibar mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad