HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 6, 2017

FANYA UTALII WA NDANI PASAKA HII KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA BEI CHEE...

Tamasha hili ni la kila mwaka na linafanyika wakati wa majira ya Pasaka watu mbalimbali kutoka Tanzania na Africa Mashariki wanaalikwa kushiriki kupanda mlima Kilimanjaro, na wengine kwenda kwenye mbuga za wanyama zilizopo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kwa upande wa mlima Kilimanjaro, ratiba pamoja na utaratibu wa kushiriki, pamoja na maelezo machache ni kama ifuatavyo:

KIPENGELE (A)*
(FULL ROUTE UHURU TREK)

6D 5N
Tarehe 9April 2017 watu watakaopanda mlima kwa siku 6 kupitia njia ya Marangu wataanza kupanda.

KIPENGELE (B)*

3D 2N
Tarehe 12April 2017 kutakuwa na watu watakaopanda mlimani kwa siku 3. Ambapo siku ya kwanza watafika kwenye kituo chao cha kwanza cha kulala (Mandara huts) ambapo jioni kabla ya dinner watatembelea Maundi crater. Na siku ya pili wataondoka kuelekea Kitu chao cha pili ambacho ni (Horombo huts) 3720Meters.

Jioni watapata fursa ya kutembelea mawe yenye rangi ya punda milia "zebra rocks" na pia jioni hiyo watakutana na wale waliopanda kwa siku 6, na kula pamoja nao mlo wa jioni, ambapo siku itakayofuatia watateremka mlimani kwa pamoja.

KIPENGELE (C)*

2D 1N
Tarehe 13April 2017 kutakuwa na watu watakaopanda mlimani kwa niku 2
Ambapo wata fika kituo cha Mandara na kupata mlo wa mchana na jioni pamoja na malazi ya usiku mmoja kituoni hapo.

Siku itakayofuata asubuhi baada ya kifungua kinywa (breakfast) watapata fursa ya kutembelea Maundi crater ambapo mchana watakutana na wale waliopanda kabla yao na baada yao.

KIPENGELE (D)*

1 DAY TRIP
Tarehe 14April 2017 kutakuwa na watu watakaopanda kwa siku moja (day trip)
Hawa wataenda hadi Mandara huts 2720 meters na kula chakula cha mchana.

Watakutana na watangulizi wao wote na baadaye kuteremka kwa pamoja hadi marangu gate na kukutana na mgeni rasmi kwa ajili ya sherehe fupi ya kukabidhiwa vyeti, pamoja na zawadi mbalimbali. Gharama ya kushiriki kwa kipengele hiki tuwasiliane.
**  ***   ****
MAHITAJI MUHIMU AMBAYO TUTAKUPATIA KWA FEDHA UTAKAZOLIPA
NI PAMOJA NA:-

- Ada zote za viingilio Hifadhini na malazi.
- Chakula kwa siku zote (Milo mitatu)
- usafiri wa kwenda hifadhini na kurudi
- usafiri wa mapokezi kutoka uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (JRO) na kurudishwa.
- vifaa vya kupandia mlimani.
- Mishahara kwa wangozaji watalii (guides)
Assistants guide, wapishi, na wasaidizi wa kubeba mizigo (porters).

Kwa mawasiliano na kujisajili, pamoja na
bei kwa kila kipengele Nipigie na au SMS kwa namba yangu hii: 0756-522-865

Sifael Malle
MD Kili Base Adventures Ltd.
E -: info@kilibaseadventures.com
W-: www.kilibaseadventures.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad