HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 14, 2017

WAZIRI MUHONGO azindua Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu mkoa wa Pwani

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.

Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.

Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg International Services.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga alieleza kuwa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu unahusisha vipengele Mradi vitatu vya utekelezaji.

Alisema kuwa kipengele cha kwanza cha utekelezaji kitahusisha kufikisha umeme kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa kabisa na miundombinu ya umeme wa gridi na kipengele cha Pili kitahusika na kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme.

“Kipengele cha Tatu katika Mradi huu kitahusika na usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi, ambayo ni vigumu kufikiwa na umeme wa gridi yakiwemo maeneo ya Visiwa”, aliongeza Mhandisi Nyamo-hanga.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.

Alisema kuwa Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Pwani utahusisha vipengele vyote vitatu na utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 204 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 30.2 ambapo utekelezaji wa sehemu ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika Machi 2019.

Mhandisi Nyamo-hanga alitoa wito kwa wananchi watakaounganishiwa umeme kukamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao mapema ili wakati mkandarasi atakapofika katika maeneo yao, wawe tayari kulipia na kuunganishiwa umeme.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo, alisema kuwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini imefanyika kwa ufanisi kwani katika mwaka 2007 ni asilimia 2.5 tu ya watanzania waishio vijijini walikuwa na umeme lakini mpaka mwisho wa mwaka 2016, upatikanji wa umeme vijijini ulifikia asilimia 49.5.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.

Alisema kuwa, Watanzania wana haki ya kujivunia miradi hiyo inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutekelezwa na TANESCO, kwani ni ya kipekee duniani kutokana faida zake kwa wananchi wa vijijini ambapo gharama mbalimbali zinabebwa na Serikali huku mwananchi akitakiwa kulipia shilingi elfu 27,000 ili aunganishiwe umeme.

Alisema kuwa, kwa kutambua umuhimu wa miradi hiyo, bajeti iliyotengwa kwa mwaka wa Fedha 2016/17 ili kusambaza umeme vijijini ni zaidi ya shilingi Trilioni moja.

Kuhusu hali ya Umeme katika mkoa wa Pwani, aliwaagiza watendaji wa TANESCO na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, kujadiliana ili kufahamu mahitaji halisi ya umeme, hasa ikizingatiwa kuwa kuna viwanda vinavyoendelea kujengwa na vilivyopo ambavyo vinahitaji si chini ya megawati 60.

Watendaji kutoka kampuni ya Steg International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.

Aidha, alitoa wito kwa wananchi kutodai fidia katika miradi ya Umeme, kutokana na umuhimu wake katika huduma za kijamii kama vituo vya Afya, Shule, majumbani na shughuli za kiuchumi ili kuleta mapinduzi katika maisha ya wananchi hao.

Wabunge pamoja na Mkuu wa mkoa wa Pwani, walipongeza juhudi za usambazaji umeme nchini zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini, chini ya Profesa Muhongo na kutumia fursa hiyo kueleza changamoto mbalimbali zinazopaswa kushughulikiwa na Serikali ili wananchi pamoja na viwanda viweze kupata umeme wa uhakika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad