HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 14 March 2017

MAKONDA AFANYA ZIARA BONDE LA MTO MSIMBAZI

 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika bonde la mto Msimbazi kukagua wakazi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na hadha ya mafuriko yaliyotokana na mvua iliyonyesha jana.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza kuvuka upande wa pili wa bonde mto Msimbazi kujionea jinsi maji yalivyofanya uharibifu kwenye eneo hilo.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na jopo la watumishi na wakazi wa jiji katika bonde la Mto Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akivuka moja ya sehemu ambazo zina maji katika bonde la mto Msimbazi
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akishuka kuelekea Bondeni kuangalia namna mvua zilizonyesha na kuleta madhara kwa wakazi eneo hilo.
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikatiza katika maeneo ya bonde la Mto Msimbazi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wajasilimali na wanawake wa bonde la mto Msimbazi ambao wanafanya biashara ya kuuzamatunda.

Na Ripota wa Globu ya jamii
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto Msimbazi kuwa mvua zinazonyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.

Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa kaitembelea maeneo hayo.
 "la kwanza katika ngazi ya mkoa kulingana na utabiri wa hali mvua zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50 maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili usema kinga ni bora kuliko tiba "Aamesema Makonda

Amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia hili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi hili kupunguza madhara. Amesema hayo yanayoonekana leo ni tabia mabaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunavyoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi la pili tunaambiwa tuhakikishe kuwa atuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad