HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 6, 2017

WAVUVI WA KIJIJI CHA NUNGWI WALALAMIKIA UVUVI HARAMU

Mwananchi Mvuvi wa Kijiji cha Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya makampuni katika ukanda wao wa bahari ya Nungwi kwa kutumia bunduki na mishare wakati wa uvuvi wao na kuwakimbiza samaki katika maeneo hayo na wao inawalazimu kwenda kuvua sehemu ya mbali na eneo hilo kutokana na samaki kukimbilia maeneo mengine, wameitaka taasisi husika kulichunguza hili ili kuepusha uvuvi huo haramu katika pwani yao.
Mwananchi wa Kijiji cha Nungwi Unguja akizungumza na waandishi wa habari kero yao kwa waandishi kutokana na kukithiri vitendo vya uvuvi haramu. 

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi wakiwa katika eneo la ufukwe wa bahari hiyo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika ukanda huo wa pwani ya nungwi wakiwa katika kazi zao za kawaida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad