HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 2, 2017

WAENDESHA BAISKELI JIJINI MBEYA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI,KUSAFIRI KWA BAISKELI KWENDA CHUNYA JUMAMOSI HII, WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI

Uongozi wa UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISES unapenda kuwataarifu kuwa maandalizi ya safari yamekamilika ambapo siku ya jumamosi tarehe 04/03/2017 tutakuwa na safari ya baiskeli kuelekea chunya Yenye umbali wa Km 70 kutoka Mbeya mjini na kurudi jumapili ya Tarehe 05/03/2017.
Tutakuwa na team ya watu 9 waendesha baiskeli na gari ya escort mpaka chunya na kisha kufanya camping, na Nyama choma (BBQ).
Tupende kutoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi bwana Festo Sikagonamo na uongozi wa shirika la ELIMISHA kwa kuweza kuunga mkono safari hii. 
Katika safari yetu tutajifunza na kujionea mambo mbalimbali ikiwemo mbeya city view point (sehemu ya kuangalizia jiji la Mbeya), local markets, barabara iliyojuu kuliko zote Tanzania, the great rift valley view point(sehemu ya kuangalizia bonde la ufa), Kona ya mkoa, Muonekano wa ziwa Rukwa kama hali ya hewa itaruhusu, mabadiriko ya uoto wa asili kati ya mbeya na chunya  maisha na shughuri za kila siku za watu wa chunya.
Kama wewe ni mwendesha baiskeli na utapenda kushiriki nafasi bado zipo na ni bure kabisa njoo na baiskeli yako tu, lakini kama utapend kushiriki kwa lengo la kutalii basi utachangia 15,000/= ikihusisha usafiri na Malazi.
Wa kwanza kulia ni Mratibu na mtu wa masoko Uyole Cultural Tourism Enterprises, katikati mwanafunzi wa mazoez kutoka Musoma Utalii Collage Musa James, na wa mwisho Mkurugenzi wa Shirika la Elimisha Bw.Festo Sikagonamo
Kushoto ni Mratibu na Muongozaji watalii Modesto Winfred Mwalingo, katikati ni Musa James na mwisho Festo Sikagonamo
Mkurugenzi wa Elimisha Festo Sikagonamo akieleza mambo mbali mbali juu ya utalii.
Kwa mawasiliano zaidi
 Piga simu namba 0783545464 au 0766422703

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad