HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 8, 2017

TOTAL, INTEGRATED WAWAKUMBUKA WANAWAKE JIJINI DAR

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Integrated Communications kwa pamoja wametoa msaada wa taa zinazotumia mwanga wa jua (sola) kwa wakina Mama wajasiliamali wa eneo la Mwananyamala jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.

Taa hizo ambazo ni za kisasa zitawasaidia wakina mama hao katika shughuli zao wakati wa usiku, kwani mara nyingi walikuwa wakitumia taa aina ya vibarati ambayo hutumia mafuta na si salama kwa afya zao kutokana na moshi wake.

Wakinamama 30 wamekabidhiwa taa hizo leo zenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano.
Diwani wa Kata ya Makumbusho, Ally Harubu akikabidhi taa ya kutumia mwanga wa jua (sola) kwa Bi. Mwajabu Mohamed mkazi wa Mwananyamala, zilizotolewa na Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Integrated Communications, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani. Hafla hii imefanyika mchana wa leo katika Viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Jamila Tindwa akizungumza jambo katika hafla ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika mchana wa leo katika Viwanja vya Mwinjuma, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania, Magreth Deodath akifafanua jambo wakati akitoa maelekezo ya namna ya kuzitumia taa hizo kwa kina mama wajasiliamali wa Mwananyamala, jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo, Jamila Tindwa
Mmoja wa wakina Mama hao akiwa na taa hizo baada ya kukabidhiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad