HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 March 2017

TFF YAMPONGEZA RAIS MPYA WA CAF AHMAD AHMAD Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limepongeza Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad kwa kufanikiwa kushinda katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika leo nchini Ethiopia.

Rais wa TFF Jamal Malinzi amempongeza na kumuahidi ushirikiano wa dhati na watakuwa pamoja katika kulisongesha soka la Afrika kwa maendeleo zaidi.

Ahmad kutoka nchini Madagascar ameshinda kwa kura 34 dhidi ya 20 za Rais  aliyemaliza muda wake Bw Issa Hayatou.     

Washindi wa CAF EXCO niFouz Lekjaa wa Morocco Billity wa Liberia,Costa wa Angola (Mmiliki wa recreativo lebolo fc),Danny Jordaan wa Afrika kusini na Amaju Pinnick wa Nigeria na Walioanguaka ni Diakite, Moucharaf na Raouraoura

Mbali na hilo, TFF pia imeipongeza Zanzibar kwa kufanikiwa kuwa mwanachama kamili wa CAF na kufikisha idadi ya wanachama 55 barani Afrika ambapo katika upigaji huo wa kura nchi 51 zilikubali kupitishwa kwa Znzibar na 3 kukataa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad