HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

BILIONI 15 ZAHITAJIKA KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA JIJINI DAR


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji.

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo kutumika tena.

Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu
itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia suala zima la uchafuzi wa mazingira.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo.

“Tupo na mpango wa kuyatumia maji taka kwa shughuli nyingine kama kilimo cha mbogamboga, unaimani kwa kufanya hivyo tutaongeza kipato cha mtu mmoja moja…Lakini ili mpango huu uweze kutimia tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kutekelezwa,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mfumo wa kutumia majitaka kwa shughuli nyingine za kibinadamu umekuwa ukitumika katika nchi zilizoendelea kama China, Israel na kwingineko ambako teklonojia hiyo imeanza.

Katika hatua nyingine Mamlaka hiyo imeanza mpango wa kufunga mita za watumiaji maji wa malipo ya kabla zinazojulikana kwa jina la ‘Lipa Maji Kadiri Unavyotumia’ (LIMAKU) ambazo tayari wamezifunga katika baadhi ya maeneo yakiwemo vikosi vya jeshi hapa nchini.

Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa wamefunga katika vikosi vya jeshi vilipo mkoani hapa pamoja na shule 20 za msingi zilizopo katika Jiji la Tanga na maendeleo yake yanaenda vizuri.

“Tumeagiza mita nyingine za Limaku zipatazo 300 hizi pia tutazifunga katika taasisi za serikali na watu wengine hasa wateja wetu wenye madeni makubwa,” alisema Mgeyekwa. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji.


Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa ambaye hayupo pichani.

Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa wakiandaa baadhi ya dondooo kuhusiana na wiku ya maji.
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wa pili kulia wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa kwenye semina hiyo.
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania,Amina Omari akuliza swali kwenye mkutano huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad