HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 3 March 2017

TAWI LA MPIRA PESA KUANZA KUFANYA USAILI WA WANACHAMA JUMAPILI

Mwenyekiti wa Tawi la mpira pesa Ustadhi Masoud Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufanya usaili wa wanachama wa tawi hilo kuanzia Machi 05.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Tawi la mpira pesa limetangaza kuanza kufanya usaili wa wanachama wa tawi hilo kuanzia Jumapili Machi 5 ili  kuhakiki wanachama na kuwapunguza hadi 250 kwa mujibu wa kanuni za klabu ya Simba.

Tawi la mpira pesa kwa sasa lina wanachama zaidi ya 750 ambao ni kinyume na kanuni za klabu hiyo ambayo inataka wanachama katika kila tawi kuwa 250.

Akizungumza na waadishi wa habari Mwenyekit wa tawi hilo Ustadhi Masoud Hassan  alisema  lengo la kufanya usaili huo ni kupunguza idadi ya wanachama ambao wengi wao walikuwa wakorofi na waliokosa nidhamu. 

"Tutataanza kufanya usaili wa kuhakiki wanachama keshokutwa Jumapili utakao endelea kwa siku sita ili kuendana na kanuni za klabu yetu ambayo inataka wanachama katika kila tawi kuwa 250" alisema Ustadh.

Masudi aliendelea kufafanua kwa kusema wanachama ambao hawatapata nafasi ya kusailiwa katika tawi hilo wataruhusiwa kwenda kufungua tawi jingine ambalo litakuwa na uongozi wake.

Wakati huo huo Ustadhi alisema hafikirii kugombea tena Uwenyekiti wa tawi hilo kwakua amelitumikia kwa muda mrefu huku akiwa na vyeo vingi.

"Sina uhakika kama nitagombea tena kwakua kwa sasa nina majukumu mengi ndani ya Simba" alisema Ustadhi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad