HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 3, 2017

MRADI WA KUKWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI UNAOFADHILIWA NA TAASISI YA MANJANO WAINGIA MBEYA

Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mbeya kuanzia Jumatatu, tarehe 8 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mbeya. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mbeya. 

Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mbeya wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mbeya waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumatatu tarehe 6 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mbeya.

Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 

Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741711 au +255 712 378516


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad