HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 8 March 2017

SUKOS YATOA MAFUNZO YA MAJANGA KATIKA KILELE CHA SIKU YA WANAWAKE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Taasisi ya Kova Foundation (Sukos) imetoa mafunzo kwa wanawake namna ya kuweza kukabili majanga mbalimbali yanayoweza kutokeza.
Akizungumza katika mafunzo kwa wakazi wa Tandale,  Mkuu wa Mikakati na Mipango wa Sukos,  Mariam Leisan amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wamemua kutoa mafunzo ya majanga kutokana na wanawake ndio waathirika wa majanga hayo.
Mariam amesema kuanza kwa mafunzo hayo eneo la Tandale ni kwasababu miongoni mwa watu waliopata majanga ikiwemo mafuriko na kushindwa kujiokoa katika sehemu salama.
Amesema wanawake na watoto ndio waathirika wa majanga hivyo wakipewa elimu ya kujiokoa katika majanga ni sawa kuokoa familia nzima pale janga linapoingia.
Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo mbalimbali juu ya wananchi kujiokoa pale yanapotokea.
Mkuu wa Mikakati na Mipango wa Sukos,  Mariam Leisan akizungumza na waandishi habari katika mafunzo ya wanawake kuhusu kujiokoa na majanga kwa wakazi wa Tandale leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Sukos, Salim Ahmedy  (Gabo Zigamba) akizungumza katika mafunzo ya wanawake wa Tandale juu ya kujiokoa katika majanga mbalimbali kwenye jamii leo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Baadhi ya wanawake wa Tandale wakiwa katika mafunzo ya kujikinga na majanga ambayo yameandaliwa na Sukos leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad