HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 March 2017

RATIBA YA ASFC YAPANGWA YANGA NA PRISONS APRILI 22

Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini limetoa ratiba ya michezo miwili ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federations Cup (ASFC) kwa timu za Yanga na Azam ambazo zilikuwa hazijapangwa.


Mechi hizo zilishindikana kuchezwa baada ya Yanga na Azam kuwa wawakilisji katika michuano ya kimataifa ambapo April 95 Azam itashuka dimbani kuvaana na Ndanda kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Yanga ambao bado wanaendelea kuiwakilisha nchi kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika wao mchezo wao utakuwa April 22 watakapovaana na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa.

Taarifa kutoka TFF zimesema kwamba michezo miwili ya mwisho ya Robo Fainali za ASFC zimepangiwa tarehe na pazia la nane bora litafungwa Aprili 22.


Tayari Simba ya Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza zimekwishafuzu hatua ya Nusu Fainali baada ya kuzitoa Kagera Sugar ya Bukoba na Madini FC ya Arusha katika Robo Fainali.

Mbao FC iliwafunga Kagera Sugar 2-1 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba wakati Simba SC iliwafunga Madini FC 1-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha bao pekee la Mrundi, Laudit Mavugo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad