HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 March 2017

NIMR NA CHUO CHA SAYANSI CHA NELSON MANDELA WATOA UTAFITI WA UGONJWA MARALE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 Utafiti unaonyesha kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa  wakikumbwa na ugonjwa marale hali ambayo usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo katika jamii hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila amesema kuwa mradi wa utafiti huo kama serikali kutafuta namna ya kuweza kudhibiti ugonjwa huo.
Amesema kuwa  mradi wa utafiti wa ugonjwa wa marale ulifanywa kuangalia mabadiliko Tabianchi na matumizi ya ardhi kwa jamii ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro na Monduli.
Dk.Neema amesema utafiti huo utasaidia kwa watunga sera wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto  pamoja Wizara ya Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi kuweza kuangalia namna ya kudhibiti ugonjwa huo ili usiwe tatizo kwa jamii ya wafugaji.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus  Mgaya amesema kuwa  mradi huo umefanywa  na NIMR pamoja na Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela katika kuangalia ugonjwa marale.
Amesema ugonjwa wa Marale kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la sahara zimekuwa zikikumbwa na ugonjwa huo hasa katika jamii za wafugaji.
Kwa upande wa Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Ugonjwa wa Marale , Profesa Paul Gwakisa  amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo wamekuja kutoa matokeo juu ya utafiti walioufanya.
Amesema ugonjwa wa marale ni tatizo kwa jamii ya wafugaji ambapo unahitaji kudhibitiwa kabla ya tatizo hilo halijawa kubwa.
 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akizungumza wakati kuzindua majadiliano ya utafiti wa ugonjwa wa marale katika Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo jijini Dar es Salaam. Kulia  ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus  Mgaya.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus  Mgaya akitoa neno katika majadiliano ya ugonjwa wa marale uliofanywa kati ya NIMR na Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela leo  jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
 Mkuu wa Mradi wa Utafiti, Profesa Paul Gwakisa akizungumza jinsi walivyofanya utafiti wa ugonjwa marale katika jamii ya wafugaji kwa Wilaya Simanjiro  na Monduli mkoani Arusha leo jijini Dar es Salaam.
 Mkutano ukiendelea
 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akiwa katika picha ya pamoja na Watafiti , Watendaji Wizara na Taasisi leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad