HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 March 2017

NGOMA, TAMBWE WAREJEA MAZOEZINI TAYARI KUWAVAA ZANACO

Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa timu inaendelea na mazoezi na wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wale waliokuwa majeruhi wamejiunga na wenzao katika mazoezi kuanzia jana tayari kwa kuwavaa Zanaco toka nchini Zambia siku ya Jumamosi..

Mwambusi amesema kuwa Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe wameanza mazoezi jana na wenzao ila mpaka sasa bado haijajulikana kama maamuzi ya benchi la ufundi kuwatumia katika mchezo wa Jumamosi wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zanaco.

"tunaendelea na mazoezi yetu na tunamshukuru Mwenyenzi Mungu baadhi ya wachezaji wetu waliokuwa majeruhi ambao ni Ngoma Kamusoko na Tambwe tayari wamerejea na kuanza mazoezi na kikosi,kiujumla wachezaji wote wana umuhimu kwenye kikosi cha Yanga hivyo kwa yeyote ambae atatumika kwa upande wetu ni sawa na hakuna tatizo,"amesema  Mwambusi.

" Zanaco ni timu nzuri na kwa sasa inajengwa upya lakini kwenye soka katika mechi yoyote ile lazima ufanye vitu viwili kwa usahihi ; maandalizi mazuri na mipango sahihi ya ushindi kimbinu na kiufundi. Kushindwa katika hayo ni kufeli,"

Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Djibout ni  Djamal Aden Abdi ambaye atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal.Kamisha katika mchezo huo Na. 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.

Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu wa Mratibu wa Mechi za Kimataifa wa Yanga Mike Mike ni Sh 20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya Rangi ya chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad