HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 1, 2017

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI AAGIZA VITUO VYA UMEME MBAGALA, KURASINI NA KIGAMBONI KUKAMILIKA MWEZI APRILI, 2017

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akiangalia eneo kutakapojengwa kituo cha kupooza na kusambaza umeme, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua vituo vya kupooza na kusambaza umeme jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara jijini Dar es Salaam ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vipya vya kupooza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini pamoja na kukagua eneo kutakapojengwa kituo cha Kupooza umeme katika eneo la Kigamboni.

Baada ya ukaguzi huo Dkt. Kalemani alieleza kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa vituo hivyo. Hata hivyo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na mkandarasi, kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika mwishoni mwa mwezi wa Aprili mwaka huu ili wakazi wa Mbagala, Kurasini, Kigamboni na maeneo ya jirani wapate umeme wa uhakika usiokatika mara kwa mara.

Aidha aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa, wanaweka uzio katika eneo kutapojengwa kituo cha kupooza umeme cha Kigamboni ili lisiingiliwe na wavamizi na hivyo kukwamisha juhudi za Serikali za kupeleka umeme wa uhakika kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia, mstari wa mbele) akizungumza katika Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua vituo vya kupooza na kusambaza umeme jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Mbagala, Mhe. Issa Ally Mangungu na wa kwanza kushoto Meneja wa Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Emmanuel Manirabona.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto mstari wa mbele) akiangalia baadhi ya nguzo za kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 katika Kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam. Pamoja naye ni wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kushoto kwa Naibu Waziri ni Meneja wa Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Emmanuel Manirabona.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kufunga miundombinu ya umeme katika Kituo cha Kupooza na kusambaza Umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad