HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 March 2017

MZUNGU WA YANGA KUKABIDHIWA MIKOBA YA KUINOA SINGIDA UNITED

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mholanzi Hans Van De Pluijm yuko mbioni kujiunga na timu ya Singinda United ambayo imepanda ligi kuu msimu ujao ikiwa ni katika kukiboresha kikosi hicho.

Timu hiyo kwa sasa ipo chini ya mwenyekiti wa kamati ya Usajili Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye amedhamiria kufanya usajili utakaokuwa na tija.

Mwenyekiti huyo ambaye ni  mshabiki wa Yanga na alionesha dhahiri kutaka kuendelea kuwapo kwa Mholanzi huyo katika kikosi cha Yanga lakini ilishindikana na tayari ameshavunjiwa mkataba na wanajangwani.

Uwamuzi wa Pluijm kwenda Singida ni moja ya mikakati ya Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili ambaye ameweka nia ya kufanya usajili wa nguvu utakaowashangaza watu wote na sio kuletewa wachezaji watakaokuwa hawana msaada na timu.

Pluijm alikaririwa akisema kuwa atasaini katika klabu moja wapo ya ligi kuu nchini hivi karibuni lakini sio Simba kwahiyo hatma yake itajulikana hivi punde tu wapi atakapoelekea mholanzi huyo na tayari ameshaonekana katika picha ya pamoja na kiungo wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe aliyesajiliwa hivi karibuni.
Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo wa kimataifa Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn FC kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni usajili wa awali.

Kutinyu anayecheza ligi ya Zimbabwe atajiunga na Singida United wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi June mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad