Mtaa Kwa Mtaa Blog

NARGIS MOHAMED NA NAFUE NYANGE WAFUNGUA DARASA LA UREMBO KWA NJIA YA DIGITALI

 Mshiriki wa Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed na Nafue Nyange wameamua kufungua shule ya urembo watakayokuwa wakitoa elimu kwa njia ya mtandao. Akizungumza jijini Dar es Salaam Nargis alisema kuwa wameamua kuandaa mafunzo hayo maalum katika fani ya urembo ili kuweza kuwawezesha wanawake na vijana waweze kujikwamua kiuchumi. 

Nargis aliongeza kuwa mafunzo hayo maalum yamewalenga watu wote na wanaweza kuyapata kidigitali, ikiwemo kwa njia ya simu au mtandao kwa gharama ya shilingi elfu kumi (10,000) tu za Kitanzania kwa mwezi. "Mafunzo hayo hayachagui jinsia; nia yetu kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye umaskini," alisema Nargis.

 Kwa upande wake Nafue Nyange aliongeza kuwa mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti ya www.glammadamlive.com
Pia anawaomba watanzania wasajili wataweza kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA, MasterCard, American Express.
Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo nia yao ya kuanzisha darasa la urembo la kidigitali. Pembeni ni Mjasiliamali Nafue Nyange. 
Mjasiliamali Nafue Nyange akisisitiza jambo. 
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget