HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 8, 2017

Mbowe amtumia ujumbe wa pole Kikwete kufuatia msiba wa mama yake mdogo

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ametoa pole kwa familia ya Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete kwa kuondokewa na mama yake mdogo.

Mbowe ameanisha hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook na Twitter kutoa pole hizo sambamba na kuwaombea kwa Mungu awape ujasiri na nguvu katika kipindi hiki.

“Natoa pole za dhati kwa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete, familia yake kwa kumpoteza mama na bibi katika wakati ambao walikuwa wakihitaji kuendelea kunufaika na matunda ya umri wake hasa hekima, busara na malezi kutoka kwa Bi.Nuru. Wakati tukimuombea kwa mola marehemu Bi. Nuru alale mahali pema kwa amani, tunaomba pia Mwenyezi Mungu awapatie ujasiri na nguvu familia ya Kikwete kuukabili msiba huu, na awafanyie wepesi katika majonzi ya kuondokewa

na mama.”

Bi Nuru alifariki Jumanne hii katika hospitali ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad