HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 8, 2017

JOKATE AWATAKA WASICHANA KUJIAMINI HILI WAWEZE KUFANIKIWA

 Jokate Mwegelo akipima afya katika zoezi liliondeshwa shule ya sekondari Manzese jijini Dar es Salaam.
 Mwanamitindo Jokate Mwegelo akizungumza na Mabinti wa shule ya Sekondari Manzese jijini Dar es Salaam juu ya kujitambua na kujiamini hili kufikia mafanikio waliyojiwekea. 
 Mratibu kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya TAI, Edith James akizungumza na mabinti wa shule ya sekondari Manzese


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mwanamitindo maharufu nchini, Jokate Mwegelo amewataka watoto kike kujiamini hili waweze kufikia mafanikio katika maisha hayo kwa kuweka juhudi katika elimu.

Jokate amesema hayo leo katika mahadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam.

“nataka niwaambie watoto wa Manzese sekondari siri kubwa ya mafanikio ni kujiamini lakini usijiamini katika ujinga hivyo mnapaswa kujiamini katika vitu vya msingi ambavyo viatweza kusaidia jamii yetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema Jokate.

Kwa upande wake program meneja wa TAI, Edith James amesema kuwa umefika wakati wa wanawake kujiamini hasa kwa kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi na usafi wa mwili kwa ujumla hasa wakati wanapokuwa katika siku zao.

Amesema kuwa taasisi ya TAI imekuwa katika kampeni kwa zaidi ya shule kumi za mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike waweze kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi.
 Picha kwa juu ikionyesha namna Jokate alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese
 Jokate akiwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese
 Daktari kutoka tasisi ya TAHMEF, Victoria Joseph  akitoa maelekezo juu ya tasisi yao inavyotoa huduma kwa watoto wa kike mashuleni
 Joakate Mwegelo akikabidhi taulo za kike kwa mmoja wanafunzi wa sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kampuni ya Kays Hygiene product Malik Mtui akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad