Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford (kushoto), akiwa na Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja wakati walipokwenda ofisi ya Balozi wa Malawi nchini.
Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Gihon, Leonce Zimbandu na Ofisa Habari, Michael Malanyingi.
Na Mwandishi, Wetu
OFISI
ya Ubalozi wa Malawi nchini imeushauri Uongozi wa huduma ya Gihon
kuwasiliana na Bodi ya usajili ya Malawi kabla ya kujaza fomu ya maombi
ya usajili wa huduma hiyo.
Lengo
ni kuutaka uongozi huo kufahamu sheria za usajili za nchini Malawi ili
kuepuka usumbufu ambao unaweza kujitokeza iwapo fomu zitajazwa bila
kuzingatia sheria na taratibu za nchi husika.
Katibu
wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama aliyasema hayo alipokuwa
akizungumza na Uongozi wa Gihon jana katika ofisi ya ubalozi huo ili
kupata ufafanuzi wa namna ya kufungua huduma hiyo nchini Malawi.
Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Gihon, Leonce Zimbandu na Ofisa Habari, Michael Malanyingi.
Alisema
ubalozi utahakikisha mawasiliano yanapatikana ili mwanasheria kutoka
bodi ya usajili ya Malawi kutoa maelekezo yanayotakiwa kufuatwa kabla ya
kufanya usajili wa taasisi (NGO).
“Unajua
mimi siyo mtaalamu wa masuala ya sheria, hivyo mawasiliano
nitakayowapatia yatafafanua vizuri kifungu cha sheria namba 5.05 cha
Malawi,” alisema.
Alisema
wajibu wa ofisi hiyo ya ubalozi ni kuwaunganisha na wenye mamlaka ili
waweze kutekeleza wajibu wao wa kisheria, hivyo hana uwezo wa tafsiri
sharia ya usajili wa NGO.
Mwanasheria
wa Huduma ya Gihon, Monica Mhoja alisema kuwa huduma hiyo imeona kabla
ya kujaza fomu za usajili wa huduma hiyo ya kiroho nchini Malawi,
waliamua kuomba ushauri kutoka katika ofisi za ubalozi huo.
Alisema
taratibu zipo tofauti kati ya nchi moja na nyingine, hivyo itakuwa
busara kufahamu sheria za usajili kutoka nchini Malawi ili kuepuka
uvunjaji wa taratibu za kisheria.
“Tunaomba
kufahamu taratibu za usajili wa NGO zilizopo nchini Malawi, kwani
tunahitaji kufungua huduma ili kufahamu mgawanyo wa madaraka ulivyo
kabla ya huduma kuanza kisheria,” alisema.
Mkurugenzi
Mtendaji wa huduma ya Gihon nchini, Rebecca Stanford alisema wamefikia
uamuzi wa kushughulikia usajili nchini Malawi baada ya watu hao
kubarikiwa huduma hiyo kiroho na kimwili.
“Tayari
tumefungua tawi la huduma ya Gihon nchini Malawi kwa muda wa miaka
miwili, hivyo kutokana na uhitaji uliopo tumeona tuisajili huduma hiyo
ili itambulike rasmi,” alisema.
No comments:
Post a Comment