HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi Ya Kuzuia Uchaguzi TLS

Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Onesmo Mpinzila pamoja na mambo mengine akipinga Kanuni za Uchaguzi za Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) za mwaka 2016.
Kesi hiyo imetupiliwa mbali baada ya Mahakama kukubaliana na hoja za mapingamizi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ndio waliokuwa wadaiwa katika kesi hiyo.
Hoja hizo ambao Mahakama imekubaliana nazo ni pamoja na kwamba mdai hakuwa na mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo na kwamba hati yake ya kiapo kilichokuwa kikiunga mkono madai yake ilikuwa na kasoro za kisheria.
Uamuzi huo umesomwa na Jaji Ignasi Kitusi kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo. Majaji wengine walikuwa ni Rose Teemba(kiongozi wa jopo) na Beatrice Mutungi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad