HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 27, 2017

ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE: WIMBO WA "WAPO" WA NEY WA MITEGO RUKSA KUPIGWA VYOMBO VYOTE, POLISI WATAKIWA KUMUACHIA HUYU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuachiwa huru kwa Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego na wimbo wake kuruhusiwa kupigwa  katika vyombo vyote vya Redio na Televisheni.

Wimbo huo unaojulikana kwa jina la Wapo  ulikuwa umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mapema na leo na yeye mwenyewe kukamatwa akiwa mkoani Morogoro alipoenda kikazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mchana huu mjini Dodoma wakati akitoa taarifa hiyo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amesema uamuzi wa kuruhusiwa kupigwa kwa wimbo umetoka kwa Mheshimiwa Rais John Magufuli baada ya kupokea ujumbe wa kumtaka hauruhusu  wimbo wa msanii huyo kupigwa katika vyombo vyote.

"Wimbo unaozungumziwa Rais Magufuli anaupenda, ameomba aachiwe huru na aendelee na kazi zake, ila anaweza uboresha zaidi wimbo wake huo kwa kuongeza vitu zaidi, kama wakwepa kodi, watumia dawa za kulevya nk". alisema Dk. Mwakyembe.

Mwakyembe alisema kuwa Rais amefurahishwa na wimbo wa msanii na kumshauri kama inawezekana aendelee kuwataja watu wengine kama vile wauza unga, wakwepa kodi, wabwia unga,wezi na wengine wasio na maadili mema katika jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad