HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 13 March 2017

COCA-COLA KWANZA YAKAMILISHA SHANGWE NA WADAU WA COCA-COLA MKOWANI MBEYA.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios (kulia),  akigongesha soda ya Coca-Cola na viongozi wengine wa kampuni hiyo  kuashiria uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji hicho mkoani  Mbeya mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha (kutoka kushoto) ni David  Karamagi - Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania, Nalaka Hettiaratchchi –  Mkurugenzi wa Mauzo wa Coca-Cola Kwanza na Gary Pay – Meneja Mkuu wa  Coca-Cola Kwanza Mbeya. Sambamba na uzinduzi wa muonekano mpya, Kampuni  ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi soko la bidhaa zake mkoani Mbeya  ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji inayotumia teknolojia ya kisasa   katika kiwanda chake kilichopo Mbeya. Picha zote na Mr. Pengo - MMG-MBEYA.
Wageni waalikwa waliofika kusherekea muonekano mpya wa kinywaji cha Coca-Cola.
---
*Yafunga mitambo ya uzalishaji ya kisasa, boresha huduma za usambazaji wa bidhaa zake
Mbeya,  Jumapili Machi 12, 2017: Kampuni ya Coca-Cola imejidhatiti kuteka zaidi  soko la bidhaa zake mkoani Mbeya ambapo imefunga mitambo ya uzalishaji  inayotumia teknolojia ya  kisasa  katika kiwanda chake kilichopo Mbeya ,  sambamba na kununua malori mapya kwa ajili ya kurahisisha usambazaji   lengo kubwa likiwa ni  kuhakikisha bidhaa zake zinapatikana katika kila  kona ya mkoa huo na maeneo mengine yote ya Nyanda za Juu Kusini.
Kutokana  na mkakati wake huu wenye mwelekeo wa kupanua soko lake, kampuni  jumamosi hii imefanya tafrija maalum ya kusherehekea  mafanikio haya   iliyofanyika katika hoteli ya  Tughimbe na kuwajumuisha wadau zaidi ya  300  kutoka sekta mbalimbali  mkoani humo, wakiwemo wafanyabiashara,  mawakala wa usambazaji vinywaji  na wanamichezo kutoka klabu ya Mbeya FC  ambayo inadhaminiwa na Coca-Cola.
Akiongea wakati wa  hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza, Basil Gadzios,  alisema  upanuzi na kufunga mitambo ya kisasa zaidi katika kiwanda cha  Coca-Cola mkoani Mbeya umefanyika  wakati muafaka ambapo umeenda  sambamba na mkakati wa kujiiimarisha zaidi katika soko la Mkoa huo na  maeneo yote ya Nyanda za Juu Kusini na kuhakikisha bidhaa zake  zinapatikana kila mahali na wakati wowote lengo likiwa na kuwawezesha  wakazi wa Mbeya kufurahia ladha murua ya kinywaji cha Coca-Cola na  bidhaa nyingine zinazozalishwa na kampuni.
“Kampuni ya  Coca- Cola inayo historia ya kuwepo mkoani hapa kwa  muda mrefu, na  tumeona ni vyema tukawashirikisha katika mkakati wetu wa mafanikio wenye  lengo la kuongeza tija na ufanisi, ambapo tumeboresha kiwanda chetu na  pia tumejipanga kusambaza bidhaa zetu kuhakikisha zinawafikia wananchi  kwa urahisi na  mkakati huu tutautekeleza katika mikoa yote vilipo  viwanda vyetu”. Alisema Bwana Gadzios.
Kwa upande wake,  Mkuu wa kiwanda hicho cha Mbeya, Gary Pay, alieleza kuwa kiwanda hicho  kimefanyiwa ukarabati mkubwa  na kufungwa mitambo inayotumia teknlojia  ya kisasa ya uzalishaji vinywaji, kujenga mabohari ya kisasa na kununua   malori makubwa ya kurahisisha usambazaji bidhaa zake kwa wateja.
Bwana  Pay alisema uwepo wa kiwanda hicho umetoa ajira nyingi za moja kwa moja  na zisizo za moja kwa moja kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya na kuongeza kuwa  kampuni imekuwa mstari wa mbele kutekeleza miradi ya kusaidia jamii,   baadhi yake ikiwa ni kutoa msaada wa madawati kwa shule za serikali na  udhamini wa timu ya mchezo wa soka ya Mbeya FC.
Alimalizia  kwa kusema kuwa kampuni itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za  kukabiliana na changamoto mbalimbali  zilizopo kwenye jamii ambapo   katika kipindi cha mwaka huu kampuni imedhamiria kutoa msaada wa  madawati 1,000 katika shule za serikali za mkoa humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad