HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 February 2017

YANGA VS NGAYA NI BUKU TATU TU, KUWAKOSA WACHEZAJI WATATU

 Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushoto) akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa marudiano na timu ya Ngaya utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, katika mechi ya kwanza Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1 nchini Comoro.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetangaza viingilio vya mechi yao marudiano dhidi ya Ngaya unaotarajiwa kufanyika wikiendi hii.

Akizungumnzia viingilio hivyo, Afisa Masoko wa klabu hiyo, Omar Kaaya amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni shiilingi 3000 kwa majukwaa ya mzunguko na viti vya machungwa,  VIP A  ni Tsh  20,000, VIP  B  ni Tsh  10,000 na VIP  C itakuwa Tsh  10,000.

Kaaya amewataka mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani ili kuishan gilia timu yao na zaidi amani inatakiwa itawale kwenye mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao.

Kwa upande wa Benchi la Ufundi wa Yanga, Kocha msaidizi wa Juma Mwambusi amesema kuwa katika mchezo huu hawatabweteka na ushindi walioupata mwazoni zaidi wanataka kuona wanapata ushindi mwingine.

Mwambusi amesema, hawatabweteka na ushindi uliopita kwani ni hazina tosha ila kila kitu inakuja na mbinu yake kwahiyo lazima tucheze kwa umakini mkubwa sana na kuweza kutokuruhusu goli.

"Tunajivunia ushindi mnono tulioupata ugenini kwani ni hazina tosha kwetu lakini tunatambua umuimu wa mchezo wetu wa marejeano ambao utafanyika siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,kikubwa nawaomba mashabiki wetu na wanamichezo wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao." amesema Mwambusi.

Kuelekea mchezo huo wachezaji watakaokosekana kwa sababu ya kuwa majeruhi ni Donald Ngoma,Amisi Tambwe na Haruna Niyonzima.
                   
Tayari Ngaya wamewasili asubuhi ya leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga ambao kwenye mechi iliyofanyika nchini Comoro Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad