
Baadhi
ya wapiga picha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiwa katika
picha ya pamoja na Rubani wa parachuti, David Eris kutoka kampuni ya HOT
AIR Safaries, mara baada ya ziara ya kuitembelea Hifadhi ya Maasai
Mara, nchini Kenya. Wapiga picha hao walitembelea hifadhi hiyo kufuatia
mualiko kwa kampuni ya kutengeneza kamera aina ya Canon ikiwa ni sehemu
ya kusherehekea kamera mpya aina ya Canon D5 Mark IV, ambapo wapiga
picha hao waliweza kupatiwa uzowefu wa kamera hiyo mpya iliyoongezewa
ubora katika upigaji picha na video pia. Mpiga picha na Blogger, Othman
Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog (wa
kwanza kulia waliopiga goti) ndiye aliyekuwa mwakilishi wa wapiga picha
kutoka Tanzania. na zifuatazo ni baadhi tu ya picha alizopiga katika
ziara hiyo.
Pundamilia akilia.
Twiga.
Balozi wa Canon na Mpiga picha maarufu Duniani, Simeon Quarrie akichukua picha mbalimbali ndani ya hifadhi ya Maasai Mara, nchini Kenya.
Duma wa Maasai Mara wakiwa mawindoni
Kanga.
Mfalme wa Pori, Simba akiwa kala pozi.
Simba jike akipanga mbinu za kwenda kuwinda wakati Dume akisubiri.
Muonekano wa vivuli vya baadi ya wapiga picha hao wakakati wa kuchomoza kwa jua.
No comments:
Post a Comment