HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 14, 2017

Wakazi wa Mwanza wazifurahia Simu za Smart Bomba

Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa ,Ayubu Kalufya akiitambulisha simu ya Smart Bomba kwa wakazi wa jijini Mwanza jana, kulia ni Mkuu wa Maduka ya Rejareja wa kampuni hiyo,Brigite Steven.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiiangalia simu aina ya Smart Bomba, wakati wa utambulisho wa simu hiyo jijini humo.
Baahi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Ziwa wakiandamana kwenye barabara ya Kenyatta jiji Mwanza jana, wakati wa kuitambulisha wa simu aina ya Smart Bomba kwa wakazi wa jiji hilo jana.
 Mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza Michael Alfred, akipokea simu aina ya Smart Bomba ikiwa ni zawadi kutoka kwa  Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa ,Ayubu Kalufya,baada ya kununua moja ya simu hizo wakati wa kuzitambulisha simu hizo jijini Mwanza.
                                                                                         
Wakazi wa jiji la Mwanza wamezifurahia simu za kisasa za Smart Bomba ambazo zilizinduliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania hivi karibuni. Simu hizo  zinazidi kuchangamkiwa na wananchi wengi hususani wakazi wa maeneo ya jiji la Mwanza na wanaozunguka mkoa huo ambapo wameshukuru kwa hatua hiyo ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo inayoendelea mkoani Mwanza, baadhi ya wananchi wamesema kuwa hatua ya kampuni hiyo kuingiza sokoni simu za kisasa za Smart Bomba zinazopatikana kwa gharama nafuu imedhihirisha dhamira ya kweli ya kampuni hiyo ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.
Bw.Focus Phabian mmoja wa wananchi ambaye amenunua simu hiyo akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa Smart Phone ni mkombozi wa mawasiliano ya kisasa kwa kuwa licha ya kuwa na unafuu wa bei pia imetengenezwa kwa kuendana sambamba na mazingira halisi ya watanzania.
“Simu ya Smart Bomba licha ya kuuzwa kwa shilingi 99,000 ambazo ni nafuu kwa watanzania wengi programu zake zinapatikana katika lugha ya taifa ya Kiswahili bila kusahau muundo wake unaowezesha kupata interneti yenye kasi kubwa ya Vodacom na kupiga picha zenye ubora wa hali ya juu .”Alisema.
“Watanzania wengi hivi sasa wana kiu ya kupata taarifa mbalimbali zinazotokea papo kwa papo na kujiunga pia na progamu za simu zinazorahisisha mawasliano kama whasap hivyo kwa Smart Bomba wengi watamudu kutumia simu za kisasa za intanenti ambazo zinauzwa kwa bei nafuu na zilizotengenezwa kwa kulenga mazingira halisi ya kitanzania”,Alisema Phabian.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya ziwa,Ayoub Kalufya,alisema kuwa tangu simu hizi ziingizwe sokoni wiki moja iliyopita kumekuwepo na mwitikio mzuri wa wananchi ambao wamekuwa wakizinunua ili  kuingia katika ulimwengu wa kidigitali.
“Smart Phone mbali na kuwa na unafuu wa bei pia inaambatana na ofa ya  mteja anayenunua simu  kuunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za bure kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom  mahali popote na wakati wowote”,Alisema Kalufya.
Kalufya aliongeza “wakati ni huu kwa wakazi wa jiji la Mwanza mikoa mingine ya kanda ya ziwa makundi kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya Smart Bomba kwa gharama nafuu na  kufurahia mawasiliano ya kisasa”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad