HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 24 February 2017

SUKARI FEKI YAKAMATWA JIJINI MBEYA,HAINA UJAZO STAHIKI NA HAIJATHIBITISHWA NA TBS |AFISA ADAI IMESAMBAA NCHI NZIMA...


Katoni ya Sukari feki ikiwa mezani ili kuonyeshwa kwa waandishi wa Habari na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya
Operesheni ya aina yake iliyofanyika maeneo ya kibiashara ya Mwanjelwa na Kabwe Jijini Mveya ikisimamiwa na maofisa wa WMA (Wakala wa Vipimo) imeibua mengi na mazito hasa kukamatwa kwa zaidi ya Tani mbili za sukari iliyochakachuliwa kuanzia Uhalali wa kuuzwa na hata Vipimo vyake.
Akiongea mbele ya Viongozi wa Mkoa na Wilaya kama Mkuu wa Mkoa Mhe.Amos Makalla na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe.William Paul Ntinika
Afisa Vipimo Bw.Deogratias M.Hussein Amesema mambo makuu waliyobaini kwenye Msako kuwa kuna Sukari wameona kwanza Kiwanda kitengenezacho hakitambuliki kisheria,hazina nembo ya ubora ya TBS na kuhusu ujazo ni tofauti.
Amesema wafanyabiashara hao wameichakachua sukari iitwayo ILLOVE wao mifuko yao imeandikwa LILLOVE na ALLOAVE ambapo katoni ya kilogramu 10 ilipimwa na kukutwa ni kilogramu 7 hivyo walaji wanaibiwa.
Jumla ya watu 14 walikamatwa na kulipishwa faini Jumla ya Shilingi Millioni 9.4.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Amos Makalla akionyeshwa sukari feki nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa na Afisa Vipimo kutoka Wakala wa Vipimo WMA.
Huu ni moja ya Mfuko wa Sukari ambazo hazitambuliki na TBS na Ujazo wake ni mdogo.
Afisa Vipimo Bw.Deogratias M.Hussein kulia akizungumzia Sakata la hiyo sukari mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe.William Paul Ntinika wa kwanza kushoto pamoja na Katibu wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Mbeya Mjini Bw.Kiwairo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad