HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 February 2017

SHULE YA MSINGI SINDE YAPIGWA KUFULI JIJINI MBEYA KUTOKANA NA KUBOMOKA KWA CHOO CHA WANAFUNZI.


Shule ya msingi Sinde iliyopo mtaa wa kagwina katika kata ya Sinde Jijini Mbeya imefungwa ghafla kutokana na Choo cha wanafunzi zaidi ya 1,600 kutitia na kubomoka hali iliyopelekea wanafunzi kukosa huduma ya choo shuleni hapo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde Mwl. Angomwile Mwanansyobe amesema kuwa Kutokana na janga hilo Jiji pamoja na Uongozi wa Shule uliamua kuifunga shule kwa kipindi cha majuma matatu ili kupisha Ujenzi wa vyoo hivyo na madarasa ya mitihani tu yaani Darasa la nne na darasa la saba ndio pekee wataendelea kusoma hapo shuleni kwa kutumia vyoo vya shule jirani ambazo zinapakana kwa ukaribu zaidi.
Mwl Mwanansyobe amesema,....."Kama Uongozi wa shule tunajua ni kwa jinsi gani taaluma kwa wanafunzi waliopo majumbani hivyo sisi kama walimu tutaitumia likizo fupi ya mwezi machi kuendelea na vipindi. 
Aidha, mara baada ya kutembelea eneo panapojengwa choo kipya tumefanikiwa kuona wananchi wazalendo hasa kina mama wakiwa wamejifunga vibwebwe kwa ajili ya kuifanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akizungumza na mwanaHabari wetu Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa choo hicho Bw.Chief  ametoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi kujitolea kwenye ujenzi huku akiulaumu Uongozi wa shule kwa ujumla kwa kushindwa kuchukua hatua za makusudi ili kutatua suala hilo la vyoo kwani tangu zamani vilikuwa vinaonekana ni kuukuu na visivyo na usalama wa kutosha. Nae ....mkazi na mzazi wa mwanafunzi ndani ya shule hiyo ametoa wito kwa wazazi kujitahidi kuitembelea shule wasomazo watoto wao ili kutambua maendeleo ya shule yao katika nyanja tofauti zikiwemo za kitaaluma na miundombinu.
Ujenzi unaendelea na Wito umetolewa kwa akina baba pia kwani wameonekana kusuasua katika zoezi hilo.
kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea kama shule......." mwisho wa kumnukuu. Aidha Mkuu huyo wa Shule ameishukuru Serikali ya Wilaya kupitia kwa Mkuu wa wilaya Mh.William Paul Ntinika, diwani wa kata ya sinde, kamati ya shule na wananchi kwa ujumla wake kwa kujitoa kwa nguvu zote kwa ajili ya kuanza ujenzi wa haraka wa choo hicho ili kuwawezesha wanafunzi kurudi shuleni kuendelea na nasomo yao.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sinde Bw.Angomwile Mwansyobe akizungumzia kuhusu kufungwa kwa Shule na changamoto zilizowakumbuka
 umoja ni nguvu Wananchi wakiendelea na kazi ya kujenga choo kipya kwa ajili ya watoto wao
 Wakina Mama kwa umoja wao na uzalendo wakisombelezea udongo ,kupunguza kifusi ili kuwarahisishia mafundi kazi ya ujenzi wa choo kipya
 Kina Mama ni jeshi kubwa,Hivi ndivyo inavyoonekana pichani huku wanafunzi kadhaa wakishuhudia wazazi wao wakichapa kazi kwa kujitolea
 Wananchi wa kata ya Sinde na maeneo jirani wakiendelea na kazi eneo kijengwapo choo kipya
 Maendeleo hayana Uchama hivi ndivyo wananchi wa vyama tofauti walivyoungana kwa pamoja
 Wakazi wa Mtaa wa Kagwina wakizidi kumiminika na kuendelea na kazi
 Viongozi wa kijiji na kamati ya ujenzi wa choo kipya wakitoa maelekezo kwa wazazi waliojitokeza kuungana na mafundi kwenye zoezi zima la ujenzi wa choo kipya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad